//
Ads

Vijana, wakinamama watakiwa kuanzisha kilimo cha biashara

Zao la Korosho
Mwandishi wetu
VIJANA na wakina mama nchini wametakiwa kujihusisha kwenye sekta ya kilimo cha biashara ili kujenga uchumi wa kaya zao na Taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bwana Francis Assenga wakati akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam.

“Vijana na wamama nchini wanatakiwa kuunda makundi ya Kilimo katika vijiji au kata zao na kuvisajili ili kuweza kupata mikopo ya riba nafuu kwani kwa kufanya hivyo kutaongeza Maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla” amesema.

Aidha Bwana Assenga amesema kuwa kwa makundi yatakayosajili  vikundi vyao na kupata mikopo kutoka Benki ya  Kilimo Tanzania, Benki itawasaidia wakulima kupata masoko pasipo kuhusisha madalali wanaowalaghai na kuwanyonya wakulima pindi wanapouza mazao yao. 


Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment