Na Mwandishi wetu
WATU
wawili, akiwemo mmiliki wa duka la dawa muhimu za binadamu katika kijiji cha
Itagata wilayani Manyoni, wanashikiliwa na Polisi mkoani Singida kwa tuhuma za
uzembe wa kusababisha kifo cha mjamzito, Heleni Maduhu (29).
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni
mume wa marehemu, Bahame Kamuda (32) na Joseph Hengwe (50) ambaye ni mmliki wa
duka la dawa katika kitongoji cha Kilulumo, kijiji cha Itagata Tarafa ya Itigi
wilayani Manyoni.
Alisema
tukio lilitokea kitongoji cha Lulanga kijijini hapo Januari 25, mwaka huu saa
9.30 alasiri wakati mjamzito huyo akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Misheni
ya Itigi kwa matibabu zaidi kutokana na kuvuja damu nyingi baada ya
kujifungulia kwenye duka la Dawa la Hengwe.
Alisema
kuwa siku moja kabla, mume wa mjamzito huyo alimpeleka mkewe kwenye Zahanati ya
kijiji Itagata ili kufanyiwa uchunguzi ambapo inadaiwa muuguzi wa Zahanati
hiyo, Grace Simon iliwaambia njia ya uzazi ilikuwa haijafunguka; hivyo
akawashauri warudi nyumbani.
Alisema
kuwa aliporejea nyumbani hali ya mjamzito huyo ikawa mbaya hivyo kumlazimu
mumewe kumpeleka Zahanati ya jirani ya Misheni katika Kijiji cha Mitundu kwa
matibabu zaidi.
Hata
hivyo, Kamanda Magiligimba alidai kuwa wakiwa njiani, mumewe aliona hali ya
mkewe inazidi kuwa mbaya zaidi, aliamua kumpeleka kwenye duka la dawa muhimu
linalomilikiwa na Hengwe lililopo jirani ambapo alijifungua mtoto wa kiume.
“Kutokana
na mjamzito huyo kuvuja damu nyingi baada ya kujifungua, mumewe aliamua kumkimbiza
katika Hospitali ya Misheni ya Itigi kwa pikipiki lakini kwa bahati mbaya
hawakuweza kufika mbali kabla ya mama huyo kufariki dunia,” alisema
Magiligimba.
0 Michango:
Post a Comment