Na Mwandishi wetu
MATOKEO ya mitihani ya kidato cha nne iliyofanyika
mwaka jana (2016) yametolewa leo ambapo shule za serikali zimeendelea kufanya
vibaya huku zile za binafsi zikipeta, anaandika mwandishi wetu.
Katika matokeo hayo jumla ya wanafunzi 277,283 ambao ni sawa na asilimia 70.09 waliofanya mitihani hiyo wamefaulu ambapo madaraja yanayohesabika kama ufaulu ni kuanzia daraja la kwanza mpaka la nne.
Miongoni mwa shule kumi zilizoongoza hakuna shuke
yoyote inayomilikiwa na serikali. Shule ya Feza Boys imeshika nafasi ya kwanza
ikifuatiwa na St. Francis Girls, Kaizirege Junior na Marian Girls huku Marian
Boys ikishika nafasi ya tano.
Matokeo hayo pia yanaonesha kuwa wavulana wamefaulu
kwa asilimia 73.26 huku wasichana wakifaulu kwa asilimia 67.06.
Katika hatua nyingine, shule sita kati ya kumi za
mwisho zimetoka katika Jiji la Dar es Salaaam.
Shule hizo ni pamoja na; Kitonga, Nyeburu, Mbopo,
Somangila, Mbondole na Kidete ambazo ni za serikali.
0 Michango:
Post a Comment