//
Ads

Lowassa akamatwa na Polisi Geita

Edward Lowassa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chadema
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chadema,  amekamatwa na Polisi mkoani Geita, kwa kile kinachodaiwa kusababisha msongamano wa watu mjini Geita.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mjini Geita, Lowassa amekamatwa baada kushuka kwenye gari lake akitokea mjini Bukoba na kwenda kununua matunda sokoni hali iliyosababisha wananchi kujitokeza kumsalimia.

Muda mchache baada ya Lowassa kuanza kusalimiana na wananchi yalitokea magari matatu ya polisi na kumchukua na kumpeleka katika kituo kikuu cha polisi mkoani Geita.

Mbali na mwingine aliyekamatwa ni Upendo Furaha Peneza ambaye ni Mbunge Viti Maalum CHADEMA  aliyekuwa katika msafara huo na Lowassa.

Mtetezi inaendelea kufuatilia tukio hilo, na itakuletea nini kinachoendelea.



Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment