RAIS John Magufuli amemteua Abdallah Bulembo aliyekuwa Meneja wa Kampeni zilizomwingiza madarakani kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Mbali na Bulembo ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi, Rais Magufuli pia amemteua Prof. Palamagamba Kabudi kuwa mbunge wa bunge hilo.
Wabunge hao wataapishwa kwa mujibu wa taratibu za bunge, ambapo linalotarajiwa kuanza vikao vyake wiki ijayo mjini Dodoma.
Mbali na uteuzi huo pia Rais Magufuli amemteua Benedicto Mashiba kuwa balozi na kituo chake cha kazi na siku atakayoapishwa vitangazwa hapo baadaye.
0 Michango:
Post a Comment