Dk. Steven Kebwe |
Na Mwandishi wetu
VYAMA vya siasa
vinavyoshiriki uchaguzi mdogo wa Udiwani katika kata ya Kiwanja cha ndege
Manispaa na mkoani morogoro vimetakiwa kudumisha Amani na utulivu.
Akitoa wito kwa uchaguzi
huo unaotarajiwa kufanyika Januari 22 mwaka huu, Mkuu wa Mkoa huo Dk. Steven
Kebwe amesema kuwa mkoa hautavumilia kuona chama chochote kinakiuka masharti ya
uchaguzi huo kwa namna yoyote ile.
Dk. Kebwe amewashauri wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki cha Kampeni na kuwataka kusikiliza maelezo yanayotolewa na vyama vyote ili waweze kuchagua kiongozi watakaye muona atafaa kuwaletea maendeleo ya kweli.

0 Michango:
Post a Comment