//
Ads

Yaya Toure: Mimi ni muislam sinywi pombe

Na Mwandishi wetu

MCHEZAJI nyota wa Ivory Coast Yaya Toure amesema hajapinga shtaka la kuendesha gari akiwa amelewa wiki mbili zilizopita.

Hata hivyo, amesema kwamba hakunywa pombe makusudi alipokamatwa akiendesha gari akiwa mlevi.

Ameandika kwenye Facebook kwamba "inafahamika wazi kwamba mimi ni Mwislamu na huwa sinywi pombe."
Hata hivyo, hajaelewa ni vipi alijipata akinywa pombe ama akajipata akiwa amelewa bila yeye kufahamu.

Yaya Toure aomba msamaha Man City
Yaya Toure: Uamuzi wa Fifa utawaumiza wachezaji
Mchezaji huyo wa Manchester City amesema: "Daima nimekuwa nikikataa pombe. Yeyote anayenifahamu na anayefuatilia uchezaji wangu atakuwa bila shaka ameniona nikikataa shampeni ya Mchezaji Bora wa Mechi kwa sababu ya kujitolea kwangu kuheshimu dini yangu."
"Ni muhimu kwangu kwamba niliiambia mahakama kwamba sikunywa pombe makusudi. Jaji akinihukumu mwenye alikubali kwamba sikuwa nimekunywa pombe makusudi."
Amesema kesi yake ilihitimishwa Jumatatu na kwamba alikubali shtaka.
"Kuendesha gari ukiwa mlevi ni kosa kubwa na ingawa sikunywa pombe makusudi, nakubali marufuku na faini na naomba radhi kwa yaliyotokea," aliongeza.


Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment