Mwanzilishi wa mtandao wa Jamii Forum, Maxence Melo akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi |
Na Mwandishi wetu
MKURUGENZI wa mtandao wa Jamii Forum, Maxence Melo, leo
ameachiwa huru baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini
wawili.
Uwamuzi huo umetolewa chini ya hakimu Godfrey Mwambapa wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es
Salaam huku wadhamini hao kila mmoja amesaini dhamana maneno ya shilingi
milioni 5.
Max ambaye ndiye mwanzilishi wa mtandao huo alishikiliwa na polisi
tangu jumanne wiki iliyopita akishitakiwa kwa makosa matatu kwa nyakati tofauti
alipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka yanayomkabili kwa Mahakimu watatu
tofauti.
Katika kesi namba 456 yenye shtaka moja ambalo amesomewa
mbele ya Thomas Simba, Hakimu Mkazi Mkuu katika mahakama hiyo na Mohamed Salim,
ambapo alidaiwa kuzuia taarifa za upelelezi wa jeshi la Polisi.
Salim amedai kuwa kati ya tarehe Mosi Aprili, tarehe 13 Desemba
mwaka huu, huko mikocheni wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaama akiwa
kama Mkurugenzi wa Kampuni ya Jamii Media inayoendesha mtandao wa Jamii
Forum alishindwa kutoa taarifa za kiuchunguzi zilizochapishwa kwenye mtandao
huo kwa Jeshi la Polisi.
Kesi nyingine namba 457 inayomkabili Melo imesomwa mbele ya Hakimu
Godfrey Mwambapa, na Mohmmed Salim wakili wa serikali amedai kuwa mtuhumiwa
kati ya tarehe 10 Mei na tarehe 13 Desemba mwaka huu huko Mikocheni, Dar
es Salaam akiwa Mkurugenzi wa Jamii Media inayoendesha mtandao wa Jamii Forum
alikwamisha upelelezi wa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za kiupelelezi kwa
jeshi la polisi
Melo anakabiliwa na kesi nyingine namba 458 mbele ya Hakimu
Victoria Nongwa, ambapo wakili wa Serikali Mohammed Salim alimsomea
mashtaka mtuhumiwa ambapo alidai kuwa alikuwa anamiliki mtandao wa bila kuwa na
kusajiliwa nchini Tanzania na kuwepewa msimbo wa (dot.tz), ambapo ni kinyume na sheria.
0 Michango:
Post a Comment