//
Ads

Sherehe za Uhuru kuhamia Dodoma


Vikosi mbalimbali vya Jeshi la Ulinzi na Usalama vikipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli


Na Mwandishi wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amesema leo ni mwisho wa kufanyika kwa sherehe za kumbukumbu ya siku ya Uhuru jijini Dar es Salaam ambapo mwakani sherehe hizo zitahamia makao makuu ya nchi, mkoani Dodoma.

Tangu Rais Magufuli kuamuru kusitishwa kwa sherehe hizo mara baada ya kuingia madarakani mwaka jana na Sherehe hizo ambazo ufanyika tarehe 9 Desemba kila mwaka zimefanyika leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza tangu Raishuyo kuingia madarakani.

“Mwaka jana niliamua tuadhimishe sherehe za Uhuru kwa kufanya usafi kwa sababu sherehe hizo zilitakiwa kufanyika mwezi mmoja baada ya mimi kuingia madarakani, nilikuwa sijakamilisha hata uteuzi wa Baraza la Mawaziri pamoja na watendaji wengine,
Lakini pia nilipouliza gharama zake nikaambiwa ni Sh. 4 bilioni ambazo niliagiza zitumike katika upanuzi wa barabara ya Ali Hassan Mwinyi ili kupunguza tatizo la foleni jijini Dar es Salaam,” amesema.

Ingawa hakutaja kiasi halisi kilichotumika katika kuandaa sherehe hizo, Rais Magufuli amesema gharama za sherehe hizo kwa mwaka huu zimepunguzwa sana tofauti na bajeti ya miaka iliyopita, ambapo alidokeza kuwa katika sherehe za mwaka huu hakutakuwa na hafla ya chakula kwa wageni waalikwa.

“Mwaka huu hakutakuwa na chakula baada ya sherehe hizi, hakutakuwa na dhifa ya kitaifa. Shughuli ikimalizika hapa uwanjani kila mtu anaenda nyumbani kwake,” amesema.
Kabla ya kuanza kutoa hotuba yake Rais Magufuli alikagua gwaride la vikosi vya kijeshi sambamba na kupigiwa mizinga 21 huku pia akishuhudia burudani ya vikundi vya ngoma, kwaya na sarakasi.


Sherehe hizo zimefanyika katika uwanja wa Uhuru ambapo zilihudhuriwa na wananchi mbalimbali, viongozi wa serikali wa sasa pamoja na wastaafu pamoja na mabalozi wa nchi mbalimbali. Zilianza rasmi saa 3:45 asubuhi na kumalizika 7:20 mchana.









Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment