Rais aliyeshindwa uchaguzi wa Gambia, Yahya Jammeh
Na Mwandishi Wetu
Kiongozi wa Gambia Yahya Jammeh amepinga matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika nchini humo mwezi huu wiki moja baada ya awali kuyakubali matokeo hayo.
Akiongea kupitia Television ya Taifa hilo Rais Jammeh alidai kwamba kulikuwa na ukiukwaji mkubwa katika zoezi la kupiga kura na kutaka kuitishwa kwa uchaguzi mpya.
Jammeh ambaye aliingia madarakani kufuatia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1994 alishindwa vibaya na mpinzani wake Adama Barrow, ambaye alishinda kwa zaidi ya asilimia 45 ya kura zote.
Barrow ambaye ni mfanyabiashara anatarajiwa kuapishwa mwezi Januari mwakani.
0 Michango:
Post a Comment