//
Ads

Aliyejifanya shilole kizimbani

Thomas Lucas Magula (21)  anayetuhumiwa kutusi watu kwa kutumia jina la Shilolekiuno_official akiwa chini ya ulinzi 
Na Mwandishi wetu
MWANAFUNZI  wa Chuo cha Bandari Thomas Lucas Magula (21)  anayetuhumiwa kutusi watu kwa kutumia jina la Shilolekiuno_official, amepandishwa kizimbani mapema leo asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni.

Sakata hilo lilizalisha vichwa vya habari mbalimbali tangu Julai 20, mwaka huu baada ya kijana huyo kukamatwa na jeshi la polisi kisha kufikishwa kwenye kituo cha Polisi Oysterbay na kufunguliwa jalada la kesi OB/RB/20932/2010 Lugha ya Matusi kwa Njia ya Mtandao.


Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment