Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli |
ZIKIWA zimepita siku 24
tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli atangaze
kuvunja Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya MapatoTanzania (TRA), Vigogo wa
taasisi hiyo wamejisalimisha kwa Mkuu huyo wa nchi, huku likimweka matatani
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Professa Benno Ndulu.
Uamuzi wa Rais Magufuli
pia unaweka njiapanda Menejimenti ya TRA inayoongozwa na Kamishna wa TRA,
Alphayo Kidata na kuwaweka katika mazingira magumu watendaji wengine wakuu
ambao wanaingia katika bodi kwa mujibu wa nyadhifa zao, akiwemo Gavana Ndulu.
Vigogo wanaoweza kujikuta
wakitumbuliwa ni Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Doto james na Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha(Zanzibar), Khamis Mussa ambao kwa mujibu wa sheria ya TRA
ya 2006 kifungu cha 16 wanaingia kwenye bodi hiyo kwa mujibu wa nyadhifa zao.
Katika hotuba aliyooitoa
kwenye mahafali ya 31 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Rais Magufuli
alisema uamuzi wa kutengua bodi hiyo unatokana na uamuzi wa chombo hicho
kuidhinisha bilioni 26 kuweka kwenye akaunti za benki binafsi.
“Tumekuta fedha kiasi
cha sh. Bilioni 26 zilizokuwa zimetolewa na TRA kwa ajili ya matumizi ya TRA,
zikapelekwa kwenye benki tatu kama Fixed deposit Account na bodi TRA ikapitisha
na ndiomaana nilipopata hizo taarifa fedha nikachukua na bodi kwa heri” alisema
Rais Magufuli.
0 Michango:
Post a Comment