Na Mwandishi wetu
MAHAKAMA imewaacha huru wataalamu wa teknolojia na mawasiliano waliotuhumiwa kusambaza matokeo ya uchaguzi Mkuu wa 2015 Kabla ya kuthibitishwa na tume ya Uchaguzi (NEC), mara baada ya upande wa mashitaka kufuta shauri hilo.
Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa mashitaka umeifuta shauli hilo mbele ya Respecious Mwijage kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kifungu cha 91(1).
Awali mshitakiwa namba saba katika kesi hiyo alifariki dunia ambaye alikuwa ni Jose Nim (51) raia wa Paris Ufaransa wengine ni Mashinda Mtei (49) mkazi wa Tengeru Arusha, Julius Mwita (40), Mkazi wa Magomeni Dar es Salaam, Frederick Fussi (25) IT, mkazi wa Mbezi Dar es Salaam, Julius Matei (45) Raia wa Kenya, Meshack Mlawa (25) Mchungaji na ni Mkazi wa Keko, Anisa Rulanyan (41) Mhandisi, Mkazi wa Kawe.
Kesi hiyo namba 267 ya mwaka 2015 yenye mashtaka matatu pamoja na kutoa taarifa za uongo kwenye mitandao wakati wakijua hazijathibitishwa.
Shitaka la pili likimkabili Julius Matei, Nimi, ambapo wanashtakiwa kuwa Oktoba 26 2015 , wakiwa katika hoteli ya King iliyopo Kinondoni , Dar es Salaam wakiwa na hati za kusafiria zenye namba A1532119, 930879 na M 27687807 walijiingiza katika ajira ya kukusanya na kusambaza matokeo ya urais ya uchaguzi wa mwaka huo ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ) bila kibali.
Shitaka la tatu lilikuwa likimkabili Julius Matei pekee yake ambaye ni raia wa Kenya mwenye hati ya kusafiria namba A1532119 akiwa ndani ya jiji la Dar es Salaam alijihusisha na biashara katika Saccos ya Wanama bila kibali.
0 Michango:
Post a Comment