//
Ads

Mahakama Dodoma kutoa hukumu ya kesi ya Kubenea

kubenea

Mahakama ya wilaya ya Dodoma, imepanga kutoa hukumu ya pingamizi lililowekwa na wakili wa mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea, katika kesi ya jinai inayomkabili katika mahakama hiyo. 
Pingamizi hilo linahusu nyongeza ya muda wa siku 60 zilizoombwa na serikali, baada ya muda awali kumalizika.
Katika kesi hiyo, Kubenea anadaiwa kumshambulia kwa mateke, ngumi na makofi, Juliana Shonza, mbunge wa Viti Maalum na sasa ambaye amepata uwaziri.
Upande wa mashitaka umeleta maombi hayo kupitia kifungu cha 225 (4) (C) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20.
Wakili wa utetezi, Isaac Mwaipopo amepinga kuwasilishwa kwa maombi hayo kwa maelezo kuwa yameletwa nje ya muda na kumetumika kifungu kisicho sahihi.
Kwa mujibu wa wakili huyo, kifungu kinachorihusu maombi ya aina hiyo, ni 225 (4) (b).
Amesema maombi ya awali ya nyongeza ya muda yaliwasilishwa mahakamani, tarehe 4 Septemba mwaka jana na hivyo tokea wakati huo, hakuna maombi mengine yoyote yaliyowasilishwa ndani ya muda.
“Mheshimiwa Hakimu, leo ni siku ya 70 tangu serikali kuisha siku 60 za maombi ya serikali. Hivyo basi, maombi haya ya leo, yameletwa mahakamani kinyume na sheria na batili,” ameleza wakili Mwaipopo.
Aliongeza: “Mahakama ni chombo huru na hivyo haipaswi kusumbuliwa na visababu visivyo na msingi. Ninaomba mahakama yako imuachie mshitakiwa na kuifuta kesi hii.”
Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkazi, James Karayemah, amepanga kutoa uamuzi wa pingamizi hilo, tarehe 18 Januari mwaka huu.
Kubenea alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza tarehe 5 Julai mwaka jana.
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu mguta

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment