OFISA Mkuu Mtendaji wa Tume ya Uchaguzi Nchini Kenya, Ezra Chiloba anatarajiwa kuchukuwa likizo ya wiki tatu na hatoshiriki katika uchaguzi wa marudio utakaofanyika wiki ijayo Oktoba 26 mwaka huu.
Taarifa kutoka ndani ya IEBC zinasema, Chiloba amefanya uamuzi huo wa kibinafsi wa kutoshiriki ili kujenga upya imani ya washikadau ambao wamelalamika kuhusu maofisa wa tume hiyo.
Ofisa huyo amekuwa chini ya shinikizo kubwa kutoka muungano wa upinzani Nasa kujiuzulu, huku mgombea wa urais wa muungano huo Raila Odinga akiitisha maandamano ya kumlazimisha kuondoka pamoja na maofisa wengine ikiwatuhumu kusimamia vibaya uchaguzi wa Agosti 8 ambapo rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi.
Matokeo ya uchaguzi huo hata hivyo yalifutwa na mahakama ya juu kwa kuzingatia sheria.
Chiloba anachukua likizo baada ya mwenyekiti wa tume hiyo, Wafula Chebukati kutaka maofisa waliotajwa baada ya uchaguzi huo wasiache kazi.
Chiloba anachukua likizo baada ya mwenyekiti wa tume hiyo, Wafula Chebukati kutaka maofisa waliotajwa baada ya uchaguzi huo wasiache kazi.
Mahakama ya juu ilisema kuwa haikupata ushahidi kuhusu makosa yaliofanywa na maofisa hao, lakini wanasiasa wamelalamika na kuishutumu tume hiyo kwa kujaribu kufanya udanganyifu katika uchaguzi huo mbali na wizi wa kura.
Uamuzi huo wa kuchukua likizo ulijadiliwa na mwenyekiti na anaamini kwamba kutokuwepo kwake hakutaathiri maandalizi ya tume hiyo kusimamia uchaguzi ulio huru na haki .
Ofisa mwingine, Dk. Roselyn Akombe amejiuzuru kazi katika tume hiyo kwa madai kwamba chombo hicho hakiwezi kufanya uchaguzi ulio huru na haki.
0 Michango:
Post a Comment