Polisi wakizuia Maandamano nchini Kenya |
Mashirika mawili ya Haki za Binadamu yameitaka serikali ya Kenya kuchunguza na kuwaadhibu maafisa wa polisi wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya watu wengi wakati wa maandamano yanayofanywa na wapinzani, baada ya uchaguzi wa Agosti nane.
Ripoti zilizotolewa na Amnesty International na Human Right Watch inawahusisha polisi na mauaji ya karibu watu karibu 70 nchi nzima, huku karibu nusu yao wakitokea mji mkuu, Nairobi.
Ripoti hiyo pia imewalaumu polisi kwa kuongeza hali ya wasiwasi kutokana na kutawanya kwake vikosi vyake katika maeneo yanayoonekana kuwa ngome ya upinzani.
0 Michango:
Post a Comment