WAHARIRI wa Gazeti la
MwanaHalisi linalomilikiwa na Mbunge, Saed Kubenea lililofungiwa na serikali
wamekanusha taarifa ya serikali kuwa gazeti hilo linaandika habari za uongo,
wamedai kuwa wao hawajawahi kuandika uongo na badala yake huandika habari kwa weledi
na ukweli.
Hayo wameyasema leo
jijini Dar es Salaam wakati wakizungumza na wanahabari baada ya gazeti lao
kufungiwa kwa muda wa miezi 24 (miaka miwili).
Aidha mmiliki wa
Gazeti hilo, Saed Kubenea amesema kampuni yake Hali Halisi Publishers,
imeiandikia barua Wizara ya Habari wakiitaka serikali kulifungulia Gazeti lao
la MwanaHALISI ndani ya siku mbili (jana na leo), vinginevyo wataenda
mahakamani kuidai serikali fidia ya Tsh. 141 Milioni kwa kila toleo.
0 Michango:
Post a Comment