//
Ads

Wengine watatu wapigwa risasi na kufariki , Nyamisati, Kibiti


Inadiwa kuwa Watu watatu wakazi wa kijiji cha Nyamisati, wilayani Kibiti wanadaiwa kufariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.

 Mkazi mmoja wa Kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina  moja la Hamza amesema miongoni mwa watu waliopigwa yumo mwanamke mmoja ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji kimojawapo kijijini hapo.

Wanaosadikiwa kupoteza maisha ni Hamid Kidevu,Yahaya Makame na Moshi Machela.

Mkuu wa wilaya ya Kibiti Gullamuhusein Kifu amesema ameliagiza jeshi la Polisi wilayani hapa kwenda eneo hilo kwa ajili ya uthibitisho.
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment