Chama cha Conservatives kitaibuka kuwa chama kikubwa mno nchini Uingereza, lakini hakitakuwa na wabunge wengi baada ya ucahguzi mkuu uliofanyika Alhamisi.
Hayo ni kutokana na ubashiri wa utafiti wa baada ya matokeo.
Utafiti huo ambao ulichukuliwa kutoka vituo vya upigaji kura kote nchini Uingereza, unaonyesha kuwa chama cha Tories, huenda kikanyakua viti 314, baada ya matokeo yote ya kura yatakapokuwa yametangazwa katika uchaguzi huo uliofanyika Alhamisi.
Kwa mjibu wa Utafiti huo, chama cha Labour huenda kikajinyakulia viti 266, kile cha Lib Dems 14, UKIP kitaambulia patupu na SNP viti 34.
Utafiti huo pia ulifanywa na kutangazwa na mashirika ya utafiti kama vile NOP/Ipsos MORI, mashirika ya Habari ya BBC/ITV/Sky pia yalibashiri.
Matokeo ya kwanza yanatarajiwa masaa machache baadaye, huku matokeo ya mwisho yakitarajiwa Ijumaa adhuhuri.
Utafiti wa matokeo hayo ya baada ya uchaguzi inaashiria kuwa chama cha Conservatives, kitakuwa viti 12 chini ya mshindi mkuu.
Inabashiri kuwa chama cha Labour huenda kikawa na viti 34, huku kile cha Conservatives kikitarajiwa kupoteza viti 17, Lib Dems kikijiongezea viti 6, ilihali SNP kikipoteza viti 22.
Kwa ujumla watu 30,450 walihojiwa, katika vituo 144 za kupigia kura kote nchini Uingereza.
Mbali na waziri wa ulinzi ambaye pia ni mwanasiasa wa chama cha Conservative, Michael Fallon kukinzana na matokeo hayo ya awali ya utafiti, pia John McDonnell wa Leba pia amesema kuwa ni mapema mno kutaka matokeo.
Mhariri wa BBC wa masuala ya kisiasa Laura Kuenssberg, anasema kuwa, ikiwa ubashiri wa matokeo hayo ya baada ya uchaguzi mkuu utathibitishwa kuwa sahihi, Waziri mkuu Bi Theresa May "atakuwa hatarini" alipocheza karata ya kuitisha uchaguzi mkuu wa mapema, ili kuboresha umaarufu wake, lakini itashindwa vibaya.
Jumla ya wabunge 650 wa Westminster wa likuwawakipiga kura na jumla ya wapiga kura milioni 46.9 waliokuwa wamejiandikisha.
0 Michango:
Post a Comment