Msanii wa muziki Shetta amekutana na rapa Chidi Benz ambaye alikuwa akisumbuliwa na matumizi ya dawa za kulevya kwa muda mrefu.
Rapa huyo amedai Chidi amebadilika kabisa kutoka katika hali ya uteja ambapo na mwili wake umerudi kama zamani.
“Baada ya kukutana naye nilimuuliza unaendeleaje sasa hivi, akasema mimi nipo poa kabisa. Pia nilipata nafasi ya kuusikiliza wimbo wake mpya ambao aliniambia anataka kuutoa. Yule ndiye Chidi Benz ambaye tunamjua kama tunavyojua hakuna mtu wakuziba pengo la Chidi Benz kwenye muziki,” alisema Shetta.
0 Michango:
Post a Comment