Kuelekea siku ya harusi ya mshambuliaji nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi na mzazi mwenzie, Antonella Roccuzzo itakayofanyika Juni 30 mwaka huu huko kwao mjini Rosario, Argentina kubeibuka minong’ono mingi baada ya Kocha Luis Enrique kukosa mualiko sherehe hizo.
Luis Enrique ambaye alitangaza kuondoka Barcelona mapema mwaka huu hajapata mualiko kutoka kwa Messi mapaka sasa huku kocha mpya wa Barcelona, Joaquin Valdes na wachezaji wote wa Barcelona wakipata mualiko.
Awali kulikuwa na tetesi kuwa beki wa Barcelona, Gerard Pique hataalikwa kwenye harusi hiyo baada ya kuvuja taarifa kuwa mke wake, Shakira haziivi na mke wa Messi ambae ni mwanamitindo maarufu nchi Hispania.
Sherehe za harusi hiyo zitafanyika katika hoteli ya Pullman ambayo tayari vyumba 250 vimelipiwa na baadhi ya majina ya wageni waalikwa yamekuwa siri.
Taarifa nyingine zimeeleza kuwa jumla ya watu 21 kutoka katika timu yake ya taifa akiwemo Aguero tayari wamelikwa na maandalizi ya harusi hiyo ya kifahari yameshaanza.
0 Michango:
Post a Comment