//
Ads

Rais Magufuli aomba fidia Nyamongo

Rais John Magufuli
WANANCHI wilayani Tarime mkoani Mara, wamempongeza Rais John Magufuli katika utendaji kazi wake na kumuomba kuingilia kati fidia ya watu waliofanyiwa tathmini ya malipo katika mgodi wa Acacia wa Nyamongo ili kuondokana na kero ya muda mrefu.


Kilio hicho walikitoa juzi  katika mkutano wa ndani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Tarime, Kemakorere na Nyamwaga ambao uliandaliwa na Katibu wa Chama hicho wilayani Tarime, Hamis Mkaruka, kufuatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na kuhudhuriwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mara, Innocent Nanzebar.

Wananchi waliofanyiwa tathmini kwa nyakati tofauti ni wa vijiji vya Nyakunguru, Kewanja na vingine kwa ajili ya kupisha maeneo yao mgodi na kufanya kazi ya kuchimba dhahabu.


Mbali na kutaka kulipwa fidia walisema walimpongeza Rais Magufuli kuunda kamati ya uchunguzi wa mchanga wa madini (makinikia) na kubainisha kuwa Serikali imekuwa ikifichwa undani wa mchanga unaosafirishwa kwenda nje.
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment