Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna
Msaidizi wa Polisi, Hamisi Issah alithibitisha jana kutokea kwa tukio hilo
ambalo limemjeruhi mwenyekiti huyo na kukimbizwa Hospitali Teule ya Misheni ya
St. Joseph iliyopo Moshi mjini.
Ingawa hakutaka kuzungumzia kwa undani ajali hiyo,
Kamanda Hamisi alisema polisi wanaendelea kufanya uchunguzi wa kina wa tukio
hilo lililotokea Machame, wilaya ya Hai.
“Ni kweli nyumba yake imechomwa moto na watu
wasiojulikana na yeye amejeruhiwa kwa moto mguuni... tuko kwenye uchunguzi
kwenye eneo la tukio,” alisema Kamishna Issah.
Alipotafutwa kwa njia ya simu kuzungumzia tukio
hilo, Mkuu wa Wilaya, Gelasius Byakanwa ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi hakupatikana kutokana na simu ya mkononi kuita bila majibu.
Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya
alisema wakati watu hao walipovamia nyumba hiyo usiku wa manane, mwenyekiti
huyo alikuwa amekaa varandani na familia yake.
"Nimekwenda kumjulia hali katika Hospitali ya
St. Joseph na amepata majeraha ya moto ambayo yamesababisha alazwe ili kupata
matibabu ya karibu zaidi," alisema.
"CCM tumepokea taarifa hizo kwa masikitiko
makubwa na tunaamini vyombo vya dola havitakaa kimya."
Alisema licha ya watu hao kukimbia baada ya
kutekeleza kusudio lao, anaamini watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
0 Michango:
Post a Comment