Klabu ya Everton inajiandaa kuja nchini Tanzania kwa ziara ya kujiandaa
na msimu ujao wa ligi ambapo wakiwa hapa wtacheza na washindi wa kombe
la Sports Pesa timu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya.
Sasa Everton wanaweza kuja na Pogba nchini Tanzania kama dili lake la
usajili kujiunga nao likikamilika kabla hawajaja Tanzania, tetesi
zinasema Everton wanajaribu kumsajili Florentin Pogba kutoka katika
klabu ya St Etienne.
Taarifa kutoka nchini Ufaransa zinasema timu za Everton na Red Bull
Leipzig zote zinapambana kumnunua mlinzi huyo wa kushoto mwenye umri wa
miaka 26 lakini Everton wanapewa nafasi kubwa kwani Florent anatamani
kucheza ligi moja na Paul Pogba.
Katika msimu uliopita wa ligi mlinzi huyo amecheza michezo 17 tu na
alishacheza dhidi ya Paul Pogba msimu uliopita katika michuano ya Europa
na jarida la Jeune Afrique limeshatabiri kwamba Florent anaweza kuitosa
Red Bull na kujiunga na Everton.
0 Michango:
Post a Comment