Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi wa Moshi limezuia utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa kuutembeza katika barabara za viunga vya manispaa hiyo, mwili aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema, Kilimanjaro, marehemu Philemon Ndesamburo .
Majibu ya barua yaliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Polisi Moshi, yamezuia mwili huo kupitishwa katika barabara za kati kati ya mji kwa kile walichoeleza kuwa leo Juni 5 na siku ya kazi na kuna shughuli za mbalimbali zinazoendelea.
Sababu ya pili iliyotolewa na ofisi hiyo ni kwamba wakiupitisha mwili huo barabarani watasababisha msongamano mkubwa ambao utakuwa chanzo cha usumbufu kwa watumiaji wengi wa barabarani.
“Ofisi ya Mkuu wa polisi wa wilaya inatoa maelekezo kuwa mwili wa Ndesamburo ukitolewa KCMC, upitishwe barabara ya YMCA kupitia Lucy Lameck Road hadi uwanja wa michezo wa Majengo ambapo kumepangwa kufanyika kwa shughuli zote za kutoa heshima za mwisho.
Jana mmoja wa wanakamati ya mazishi ya Ndesamburo, Anthony Komu aliliambia Mwananchi kuwa mwili wa Ndesamburo utachukuliwa KCMC saa 4 asubuhi na kupitishwa katika barabara kuu za mji wa Moshi ili kuwawezesha ambao hawatapata nafasi ya kufika Majengo, kuuaga mwili huo.
0 Michango:
Post a Comment