Mahakama ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi imemhukumu kwenda jela miaka 23 mkazi wa kijiji cha Kalovye, Osward Mpalasinge (26).
Amepewa adhabu hiyo baada ya kupatikana na hatia ya kuvunja na kuiba vitu mbalimbali ikiwemo cheti cha kidato cha nne. Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Teotimus Swai baada ya mshtakiwa kukiri kosa mahakamani.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Swai alisema mtuhumiwa amekutwa na hatia pasipo shaka hivyo anahukumiwa kwenda jela miaka 23.
Awali, Mwendesha Mashitaka, Baraka Hongoli alisema mshitakiwa alitenda makosa ya kuvunja na kuiba Mei 25 mwaka huu saa mbili usiku nyumbani kwa Veronica Crispin katika Kijiji cha Kalovye, Inyonga.
Alidai kwamba mshitakiwa alifika nyumbani hapo, akavunja na kisha kuiba nguo zenye thamani ya Sh 110,000 na cheti cha kidato cha nne cha Henreth Edward Kalamu, kilichotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) mwaka 2015.
Hongoli aliitaka mahakama kutoa adhabu kali kwa mtu huyo ili iwe fundisho kwa kuwa wizi wa aina hiyo ndio umesababisha usumbufu na watu kupoteza ajira zao serikalini na maeneo mengine pindi uhakiki wa vyeti unapofanyika.
Akijitetea, mshitakiwa aliiomba mahakama impatie muda ili aweze kwenda Dar es Salaam kumtafutia mtu huyo cheti kingine
0 Michango:
Post a Comment