Moja ya Changamoto zinazo mkabili Rais mstaafu, Jakaya Kiwete kwenye shughuli za kilimo cha Mananasi ni Upatikanaji wa Maji ya kutosha.
Hayo ameeleza leo alipotembelewa na Mwenge wa Uhuru kwenye shamba lake la mananasi lenye ukubwa wa eka zaidi ya 200 mkoani hamo,
Amesema ingawa kilimo alianza tangu mwaka 1989, lakini suala la palizi na ukosefu wa maji ni moja ya changamoto anazokabiliana nazo.
JK amesema kuwa ameanza kilimo miaka mingi na mpaka anastaafu ailikuwa anaendelea na kilimo, huku akikabiliwa na changamoto ya palizi hususan kwenye mananasi unaweza kupalilia zaidi ya mara tatu.
Amesema kuwa ingawa mananasi yanazaa vizuri kama yatapata huduma zote kikamilifu, lakini mkulima anaweza kupambana na ukosefu wa masoko pindi unapofikia msimu wa mavuno.
"Hata kama viwanda vitajengwa kwa wingi lakini ili mkulima apate faida ya juu ya kilimo hasa cha mananasi ni lazima kuwe na bei nzuri, lakini kama wanunuzi watakuwa wananunua bei isiyo na masilahi hakutakuwa na maendeleo kwa wakulima,"amesema.
Amesema kuwa mikakati aliyonayo kwa kushirikiana na taasisi na wakulima mbalimbali ni kutafuta mbegu za mananasi kutoka nje ya nchi na mkakati wa kuanzisha kilimo cha mananasi kwa njia ya umwagiliaji hali aliyosema itawainua wakulima wengi na kujikwamua katika janga la umaskini.
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa, Amour Hamad Amour amempongeza Kikwete kwa kuonyesha mfano bora hususan kuendeleza kilimo cha mananasi huku amiwahimiza Watanzania kuiga mfano huo.
0 Michango:
Post a Comment