JESHI la polisi katika wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga linamshikilia baba mmoja wa miaka 55 kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake mwenye umri wa miaka 6 na kumsababishia maumivu makali.
Kwa sasa mtoto huyo amelazwa katika hospital ya wilaya ya kishapu akipatiwa matibabu. Baba huyo alimbaka mtoto wake akitekeleza maagizo ya mganga wa kienyeji ili kupata utajiri. Mganga huyo pia anasakwa na jeshi la polisi.
Mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa ya Tanzania iliyo na idadi kubwa ya watoto wanaolawitiwa, kupigwa na kubakwa.
0 Michango:
Post a Comment