//
Ads

Kilwa yahofia kupoteza Mapato

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi inahofu ya kupoteza mapato yake ya ndani iwapo zao la ufuta litaingizwa na kununuliwa kwa mfumo wa stakabadhi za mazao ghalani katika wilaya na halmashauri hiyo. Hofu hiyo ilielezwa juzi na baadhi ya washiriki waliotoka katika halmashauri na wilaya hiyo walikuwepo kwenye kikao cha wadau wa zao la ufuta wa mikoa ya Lindi na Mtwara kilichofanyika juzi katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Abou Mjaka huku akionesha ushahidi wa jinsi mfumo huo ulivyo shindwa kuinufaisha halmashauri hiyo kwa muda wa miaka mitatu mfululizo, tofauti na mfumo wa soko huria.
Mjaka ambae maelezo yake yaliungwa mkono na diwani wa kata ya Kivinje Singino, Jafari Arobaini. Alisema hiyo hautakuwa mara ya kwanza mfumo huo kutumika katika wilaya hiyo. Hata hivyo uliosababisha kutofikia makisio ya mapato yanayotokana na ushuru wa zao hilo. Badala yake yalishuka.
“Hali hiyo nitofauti na mfumo wa soko huria ambao kila mwaka tulivuka lengo letu tulilokuwa tunakisia”. Alisema mfumo huo ni mzuri na manufaa kwa wakulima.
Hata hivyo hauna budi kutumika katika maeneo yote inayolima zao hilo kama ilivyo korosho. Huku alibainisha kuwa iwapo mikoa mengine, hasa mkoa wa Pwani ambao mpaka wake na mkoa wa Lindi upo katika wilaya hiyo hakutakuwa na faida kwa halmashauri hiyo.Kwasababu wakulima hawatakubali kusubiri malipo kama walivyosubiri malipo ya korosho wakati mkoa wa Pwani utakuwa unanunuliwa kwa fedha tasilimu.
Changamoto nyingine ambayo itakwamisha nia njema ya serikali kwa wakulima aliyoitaja mwenyekiti huyo ni zao hilo na nafaka nyingine kutokuwa na bodi. “Hatupingi wala kubeza mfumo huu bali changamoto hizo ziondolewe kwanza kabla ya kuanza kutumika,” alisisitiza Mjaka.
Nae Arobaini alisema mfumo huo hauna budi kutolewa baada ya wakulima kupewa elimu ya kutosha badala ya kuingiza na kuanza kutumika. “Hata mnaposema tusimamie wakulima wasiuze kwa walanguzi au wasipeleke ambako hautanuliwa kwa mfumo huo hatutaweza kuwazuia hao wakulima wa zao hilo wapo wengi hawalingani ni idadi ya sisi viongozi. Lakini kama alivyosema mwenyekiti wangu mfumo huo ulishatutia hasara watu walikuwa wanachukua vibali maeneo mengine lakini ufuta wanachukua Kilwa, sisi sio wageni wa mfumo huo tukitaka tufanikiwe maeneo yote yanunue kwa mfumo huo, “ alisema Arobaini.
Hata hivyo aliyekuwa mwenyekiti mwenza wa kikao hicho, mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego aliwataka viongozi kutotengeneza mazingira ya kukatisha tamaa mipango ya serikali dhidi ya wananchi. Badala yake wawe bega kwa bega na serikali kwa ajili ya kufanikisha nia njema kwa wananchi wake. Ambapo uzalendo na utayari wa viongozi kuwapigania wananchi unahitajika sana.
Nae mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi akiwaonya wanasiasa kuacha kukwamisha maagizo na mipango ya serikali kwa wananchi kwa ajili ya kulinda masilahi yao binafsi. Huku akionya hawatakuwa na muhali wala simile na viongozi yeyote ambae kauli, vitendo na mienendo yao itathibitika dhahiri wanashiriki kuwadhulumu wakulima. “Tumepewa mamlaka ya kusimamia mambo yote katika mikoa hii, kwahiyo hatutakuwa tayari kuona kiongozi yeyote anavuruga mipango ya serikali. wakuu wa wilaya na kamati zenu za ulinzi na usalama hakikisheni mnasimamia kikamilifu zoezi hilo,” alisisitiza Zambi.
Licha ya wasiwasi uliooneshwa na washiriki hao wa wilaya ya Kilwa, washiriki wengine waliotoka katika wilaya zote za mikoa hiyo waliliridhia mfumo uanze kutumika kununulia zao hilo la ufuta msimu huu wa 2017/2018
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment