//
Ads

Hiki ndio kisiwa ambacho wanawake hawaruhusiwa kufika

Kisiwa  cha Okinoshima
JOPO moja la ushauri limependekeza kisiwa kimoja nchini Japan, ambapo wanawake hawaruhusiwi kufika, kitambuliwe kama turathi ya ulimwengu.
Kisiwa hicho cha Okinoshima huchukuliwa kuwa kitakatifu kaisi kwamba ni wanaume pekee wanaoruhusiwa kuzuru, gazeti la Asahi Shimbun linasema.
Na hata wanapofika huko, hawaruhusiwi kuondoka na chochote, hata kipande cha nyasi.
Jopo hilo limependekeza Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) litambue kisiwa hicho kama turathi ya ulimwengu. Uamuzi unatarajiwa kufanywa katika mkutano wa Unesco mwezi Julai.
Katika kisiwa hicho, kuna madhabahu ya Munakata Taisha Okitsumiya, ambayo ni ya kumtukuza miungu wa baharini.
Katika kisiwa cha Okinoshima, kuliandaliwa matambiko kwa ajili ya usalama wa meli na pia wakazi wa Japan walitumia kisiwa hicho kuwasiliana na wakazi wa rasi ya Korea na China kati ya karne ya nne na tisa, gazeti la Japan Times linasema.
Bado kuna miiko kuhusu kisiwa hicho, mfano wanawake kupigwa marufuku.
Wageni wa kiume pia hutakiwa kwanza kuvua nguo zao zote na kufanya tambiko la kujitakasa.
Aidha, hawatakiwi kufichua chochote kuhusu waliyoshuhudiwa wakiwa kwenye ksiiwa hicho.
"Haya ni baadhi ya mambo ambayo itabidi yazingatiwe iwapo kitaorodheshwa kuwa turathi," anasema Asahi Shimbun, na kueleza kuwa huenda kisiwa hicho kikawa maarufu sana kwa utalii.
Hata hivyo, bado hakuna uwezekano kwamba amrufuku dhidi ya wanawake itaondolewa.
"Msimamo wetu kuhusu jinsia hautabadilika hata kama kitaorodheshwa kuwa Turathi ya Ulimbwengu," afisa wa Munakata Taisha aliambia gazeti la Mainichi Daily, "Tutadhibiti watu wanaozuru kisiwa hicho."
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment