Na Mwandishi
Wetu
ZITTO
Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini ametoa maoni yake katika ukurasa wake wa mtandao
wa kijamii wa Facebook kuhusu hali ya chakula inavyopendelea nchini ikiwa
pamoja na suala la chakula nchini.
Hiki
hapa chini alichokiandika:-
Serikali ina kauli mbili
zinazokingana juu ya hali ya chakula nchini
Siku
nzima ya jaa nilikuwa natakiwa na waandishi wa Habari kutoa maoni yangu kuhusu
uteuzi wa Mtanzania mwenzetu, na mke wa Rais aliyepita, Mama Salma Kikwete kuwa
Mbunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
Niliwaambia
sina maoni yeyote. Leo baada ya magazeti kuandika maoni ya watu mbali mbali
nimeulizwa tena. Jibu langu, ambalo ninaliweka hapa kwa umma, ni kwamba Mama
Salma Kikwete ana haki zote kama Mtanzania mwengine yeyote kuteuliwa ama
kuchaguliwa Kwa mujibu wa Katiba yetu. Hivyo uteuzi wake kwa maoni yangu ni
kama teuzi nyengine zozote zile.
Kuolewa
kwake na aliyekuwa Rais hakumwondolei yeye haki zake za kikatiba. Kama mwenyewe
ataridhia ninamtakia kila la kheri katika kazi yake mpya. Sababu za kuteuliwa
kwake anajizuia aliyemteua na baadhi ya wasomi wabobezi Kama Prof. Kitila
Mkumbo wamenukuliwa wakifanya uchambuzi mzuri Kabisa kwenye gazeti la The
Citizen la Leo.
Kwangu
Mimi, kwa maoni yangu, nchi yetu inakabiliwa na mambo makubwa zaidi ya kujadili
na kutolea maoni ikiwemo suala la njaa. Serikali kwenye suala hili la njaa
imeyumba sana na kwa kiasi flani imewayumbisha pia wananchi wanyonge
wanaokabiliwa na tatizo hili, na kwa maoni yangu naamini kabisa Serikali
haijatekeleza wajibu inavyostahili. Kama mzalendo kwa taifa langu nachukua
wajibu wangu kuonyesha mapungufu hayo ya Serikali pamoja na kutoa njia mbadala.
Jana,
Serikali kupitia Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea
kusisitiza kuwa haitatoa chakula cha msaada kwa Watanzania watakaokabiliwa na
njaa. Rais alisema "tumezoea kuambiwa maneno matamu matamu kwamba hakuna
mtu atakeyekufa kwa njaa. Mimi nawaambia usipolima utakufa na njaa".
Serikali
kwa kauli za namna hii inawachanganya watanzania, kwanza ni muhimu sana kujua
(na naamini Serikali inajua) kuwa wananchi hawa wamelima, suala la hali ya njaa
si kwa sababu ya kutokulima kwao, bali ni kwa sababu kadhaa zilizo nje ya uwezo
wao, ikiwemo hali ya hewa yenye mvua chache.
Mfano
mikoa ya Singida, Shinyanga na Tabora wananchi wetu walilima, lakini mvua
hazikunyesha kabisa, mahindi yalikauka na majaruba ya mpunga hayakuwa na maji
kabisa kati ya mwezi Desemba na Januari ambacho ndio kipindi cha msimu wa
Kilimo kwa mikoa hiyo. Sasa Serikali kupitia Rais inapowaambia wananchi kuwa
'wasipolima watakufa na njaa' si sawa, ni kama vile tunaihusianisha njaa na wao
kutolima, jambo ambalo si kweli.
Rais
wetu sio tu ni Amiri Jeshi Mkuu wa Taifa letu (Commander In Chief) bali pia
anapaswa kuwa Mfariji Mkuu (Comforter In Chief) kwa watu wetu katika nyakati za
majanga kama matetemeko ya ardhi, mafuriko na ukame ambao unasababisha njaa.
Kazi
kuu ya Serikali yoyote ni ugavi wa matumaini kwa wananchi, na Rais wa nchi
anapaswa kuwa Kiongozi wa kugawa matumaini hayo, hatusemi serikali itoe
matumaini hewa, lakini pia hatukubali serikali 'ivunje moyo wananchi' kwa
kuhusisha hali ya ukame na wao kutokulima. Hili si sawa.
Januari
31, mwaka Serikali ilitoa tamko juu ya suala la njaa, tamko husika lilitolewa
na Waziri wa Kilimo, Chakula na Uvuvi, kwamba kuna Halmashauri 55
zinazokabiliwa na njaa na kwamba Serikali itapeleka chakula cha bei nafuu ili
kuhakikisha kuwa wananchi katika Halmashauri hizo 55 hawafi njaa. Serikali hapa
ilichukua jukumu lake la kutoa matumaini kwa wananchi hawa.
Waziri
wa Kilimo, Chakula na Uvuvi ni mteule wa Rais, ni sehemu ya Serikali hii, sasa
mkuu wa Serikali husika anaposema kuwa 'watu walime na hakuna chakula cha
msaada' anafuta matumaini haya, na si tu kufuta matumaini kwa wananchi lakini
pia anawachanganya wasaidizi wake ambao wanaweza kuogopa kutekeleza msimamo wa
Serikali uliotolewa bungeni na Waziri wa Kilimo, Chakula na Uvuvi wa kupeleka
chakula cha msaada katika Halmashauri hizo 55.
kuogopa
kupeleka chakula maeneo yenye njaa na hivyo kusababisha watanzania kupoteza
maisha. Ninarudia kauli yangu kwamba iwapo Mtanzania yeyote atakufa kwa njaa
hatutakuwa na budi kumwajibisha Rais kwa kutumia Katiba.
Utafiti
wa Shirika la TWAWEZA wa mwezi Februari 2017 unaonyesha kuwa Theluthi ya
Watanzania ( Watanzania 17 milioni) Hivi sasa wanalala njaa ama kushinda na
njaa. Pia nusu ya Watanzania wanakabiliwa na upungufu wa chakula. Hawa
wanahitaji matumaini kutoka kwa Serikali na sio taarifa mbili tofauti za
Serikali zinazojikanganya.
Ni
muhimu wananchi waelewe kuwa suala la njaa na ukame si jipya nchini, mwaka 2006
na 2007 nchi ilikumbwa na ukame mkubwa sana na Rais wa wakati huo alitamka kuwa
"hakuna Mtanzania atakayekufa kwa njaa". Tuliona Serikali nzima chini
ya kiranja wao, Waziri Mkuu ikizunguka nchi nzima kuhakikisha kuwa 'hakuna
Mtanzania anakufa kwa njaa'.
Kwanini
Serikali ilifanya hivyo mwaka 2006/7? Ni kwa sababu KATIBA inatamka kuwa kila
Mtanzania ana haki ya kuishi na ni wajibu wa Serikali kuhakikisha kuwa haki hii
ya kuishi inalindwa. Ndio maana Serikali ilianzisha Wakala wa Akiba ya Chakula
(NFRA) kwa lengo la kuhakikisha tuna akiba ya chakula cha kutosha, na kwamba
ikitokea kuna majanga ya asili kama ukame basi 'Mtanzania hafi kwa njaa'.
Naiasa
Serikali itekeleze wajibu wake huu wa Kikatiba - ihakikishe hakuna mtanzania
anayekufa kwa njaa. Kushindwa kufanya hilo ni kushindwa kulinda Katiba.
Kabwe Z.
Ruyagwa Zitto
Mbunge -
Kigoma Mjini
Kigoma
Machi 3,
2017
0 Michango:
Post a Comment