Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (mwenye kofia) akiangalia ramani ya ardhi hiyo aliyopewa wiki iliyopita. Picha ndogo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.
Na Mwandishi
Wetu
WAZIRI
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameingiria kati mpango
wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kukabidhiwa ardhi kwa ajili ya
kujenga viwanda, kwani alidanganywa na aliyempatia.
Lukuvi
amesema Makonda alidanganywa na mfanyabiashara, Mohamed Ikbar kuwa ardhi hiyo
ni mali yake, huku akijua kuwa ni mali ya serikali.
Makonda (katikati) akikagua ardhi aliyopewa. Kulia mfanyabiashara, Mohamed Ikbar
Waziri
huyo amesema serikali itachukua hatua kali za kisheria dhidi ya mfanyabiashara
huyo kwani alifanya kitendo hicho makusudi kwa malengo yake binafsi.
"Sitaki
ardhi itumike kama sehemu ya wafanyabiashara kutakatisha fedha chafu" amesema
Lukuvi.
0 Michango:
Post a Comment