Zitto Kabwe, akiwa na Tundu lissu Mahakama ya kisutu |
LEO Tundu Lissu na Wahariri wa Gazeti la Mawio, Jabir Idrisa
na Simon Mkina wanaendelea na kesi inayowakabili.
Januari 12 hadi 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam,
washitakiwa watatu, Jabir, Mkina na Lissu, kwa pamoja waliandika na kuchapisha
taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja
Zanzibar’.
Katika shtaka la pili alidai washatakiwa ,
Januari 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, walichapisha habari hizo
ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.
Shtaka la tatu linamkabili mshtakiwa wa tatu, Mehboob
ambaye anadaiwa kuwa Januari 13 katika jengo la Jamana lililopo Manispaa
ya Ilala, Dar es Salaam, alichapisha gazeti la Mawio lililokua na taarifa
za uchochezi.
Alidai mshtakiwa huyo pia alichapisha gazeti hilo bila
ya kuwasilisha hati ya sheria ya kiapo kwa Msajili wa Magazeti.
0 Michango:
Post a Comment