Na Mwandishi wetu
WAJUMBE wa Kamati ya
Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wameeleza kushangazwa
kushindwa kufanya kazi miradi mikubwa kutokana na kukosekana kwa umeme.
Mweyekiti wa Kamati
hiyo Mhe. Hamza Hassan Juma ametoa kauli hiyo kutokana na uwanja wa Ndege
kisiwani Pemba kwa baadhi ya kazi kusimama kutokana na kukosekana kwa umeme wa
uhakika.
Amesisitiza
kuwa haiwezekani kwa Serikali, wizara zinazohusika na uongozi wa uwanja huo
kushindwa kutafuta transfoma maalum uwanjani hapo ili kuruhusu miradi mikubwa
iliyopo iweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Akizungumzia
suala hilo, Naibu Waziri wa ujenzi mawasiliano, na usafirishai Zanzibar
Mohameda Ahmad ametoa rai kwa viongozi wa uwanja huo kujenga utamaduni kukutana
na viongozi husika ili kutatua changanmoto zinazowakumba na sio kufanya mambo
kienyeji enyeji.
Akitoa taarifa meneja wa Mamlaka ya viwanja vya ndege Pemba
Rajab Ali Mussa, amesema kwa mwaka 2016 jumla ya abiria laki 1, mia moja 83
walihudumiwa ambapo kati yao abiria 50 elfu, mia 9 na 94 walishuka huku abiria
49 elfu, mia 1 na 89 wakiondoka.
0 Michango:
Post a Comment