Katibu wa idara ya itikadi na uenezi CCM Zanzibar Bi Waride Bakari Jabu |
Na Mwandishi wetu
WAKATI
chama cha mapinduzi CCM kikiwa kwenye shamrashamra za kuelekea miaka 40 tangu
kuanzishwa kwake, katibu wa idara ya itikadi na uenezi CCM Zanzibar Bi Waride Bakari Jabu amesema maadhimisho hayo yatafanyika katika ngazi za mikoa.
Akizungumza na waandishi wa habari Afisi kuu ya CCM Kisiwandui
mjini Zanzibar, Bi. Waride amesema kila mkoa ulishaandaa ratiba za shughuli
zitakazofanyika katika mikoa yao pamoja na kuwepo kwa zoezi la usafi wa
mazingira.
Amezitaja shughuli nyengine kuwa ni kuwakagua wangonjwa na
kuwafariji wazee wasiojiweza, mikutano mikuu ngazi mbali mbali, zoezi la
kupanda miti katika maeneo mbali mbali ya kijamii na vyanzo vya maji pamoja na
michezo na makongamano yatakayoeleza historia ya CCM na mafanikio
ya chama hicho katika kipindi cha miaka 40.
Pamoja na hayo amesema chama cha mapinduzi kinawashukuru kwa
dhati kabisa wana CCM na wananchi wote wa jimbo la Dimani pamoja na
kata za mikoa ya Tanzania bara iliyofanya uchaguzi kwa kupiga kura kwa utulivu
na kukipa chama hicho ushindi mkubwa.
Chama cha mapinduzi kimezaliwa Februari 5 ya mwaka 1977 baada ya
kuungana kwa chama cha TANU na ASP.
0 Michango:
Post a Comment