![]() |
Meneja Mfumo wa Kieletroniki wa Dirisha Moja la Huduma, Tinka Felix akizungumza kuhusu mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window System). |
Na mwandishi wetu
KATIKA kuhakikisha
inaboresha huduma kwa wafanyabiashara ambao wanaingiza mizigo nchini kwa njia
ya bandari, mipaka na viwanja vya ndege, Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato
nchini (TRA) imeeleza mpango wa Serikali ya kuanza kutumia mfumo wa Dirisha
Moja la Huduma (Electronic Single Window System).
Mfumjo huo ambao umeelezwa
kuwa utamaliza tatizo la mizigo kukaa muda mrefu bandalini kwa sababu ya
kukosekana vibali.
Akizungumza na
waandishi wa habari baada ya kumalizika mafunzo ya siku moja kuhusu mfumo huo kwa
taasisi zinazotoa vibali na wafanyabiashara, Meneja Mfumo wa Kieletroniki wa
Dirisha Moja la Huduma, Tinka Felix amesema lengo la kuanza kutumia mfumo huo
ni kuboresha huduma ambazo wanazitumia sasa ili wafanyabiashara wanaoingiza
mizigo nchini waweze kuipata kwa haraka kuliko ilivyo sasa.
“Ni mpango wa Serikali
kuboresha huduma kwa wateja kwa kupunguza muda wa kutoa mizigo bandarini au
mipakani au kwenye viwanja vya ndege, kupitia mfumo huu wateja hawatakuwa
wakienda kwenye idara na taasisi za Serikali na badala yake wakiwa hukohuko
kwenye ofisi zao wataweza kuomba na kupata vibali na kupata bili za malizo
kwenda kulipa benki, mfumo pia utafanya kazi na benki," amesema Felix.
Amesema Tanzania
haitakuwa nchi ya kwanza kutumia mfumo huo na mataifa mengi yanautumia ili
kurahisisha huduma kutolewa kwa haraka kwani mfumo wa sasa wa forodha (tancis
system) unashindwa kufanya kazi kwa haraka jambo ambalo linasababisha mizigo
kuchelewa kutolewa kutokana na muda mrefu mmiliki kutumia kutafuta vibali.
0 Michango:
Post a Comment