![]() |
Yahya Jammeh |
Na Mwandishi wetu
MSHAURI maalumu wa Rais wa Gambia Adama Barrow amesema zaidi ya dola za Kimarekani
milioni 11 zinaaminika kutoweka katika hazina ya serikali, kufuatia kuondoka
madarakani kwa mtawala wa muda mrefu Yahya Jammeh.
Mia Ahmad Fatty amewaambia Waandishi
wa habari katika mji mkuu wa Senegal Dakar kwamba wataalamu wa masuala ya fedha
wanatathmini kujua ni kiasi gani kwa sasa kimepotea.
Amesema Gambia kwa sasa ina tatizo
kubwa kifedha kwa hazina yake kutokuwa na kitu.
Habari zinasema magari ya kifahari
na mali nyingine zilionekana zikipakiwa katika ndege ya mizigo ya Chad kwa
niaba ya Rais Jammeh siku alipoondoka nchini humo.
Maelfu ya watu walikusanyika katika
Ikulu ya nchi hiyo jana jioni wakiyaangalia majeshi ya Senegal yakiingia kwa
ajili ya kuweka usalama kabla ya kurejea nchini kwa Adama Barrow.
Rais Barrow yupo nchini Senegal na
bado haijulikani ni lini hasa atarudi Gambia na kuingia ofisini.
Alisema atarejea tu baada ya
kuhakikishiwa usalama wake.
0 Michango:
Post a Comment