//
Ads

Waliomchoma mkuki mkulima mbaroni morogoro

Augustino Mtitu (35) aliyechomwa na mkuki mdomoni na kutokea shingoni
Na Mwandishi wetu

WATU 12 wametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi mkoni Morogoro kwa tuhuma za kumjeruhi Augustino Mtitu kwa kuchoma mkuki mdomoni na kutokeza shingoni katika eneo la Mikumi Wilayani Kilosa mkoani humo.
  
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa Ulrich Matei watuhumiwa hao walikamatwa na silaha 3 ambazo ni 1 aina ya AK 47, 2 aina ya shotgun, magazine3 na risasi 19 za AK 47 pamoja na risasi 4 na shotgun moja zinazomilikiwa kinyume na sheria kufuatia Askari polisi kupata taarifa za kiintelijensia za umiliki wa silaha kinyume na sheria na kufanya msako maalum mara baada ya mtu huyo kuchomwa mkuki.

Kamanda Matei amesema kuwa  desemba 24 saa 1 usiku katika kata ya Mang’ula wilayani Kilombero walifanikiwa kukamata silaha aina ya AK 47 no.KO 363394ikiwa na magazine 3, moja ikiwa na risasi za AK 47 19 ikiwa imehifadhiwa kwenye begi ambayo waliipata nyumbani kwa mwanamke mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja kufuatia kukimbia mara baada ya kuona askari wakielekea nyumbani kwake.

Amesema kuwa siku hiyo hiyo majira ya saa 11 alfajiri katika kata ya kidodi polisi hapo pia walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja ambaye anakadiriwa kuwa na miaka 54 mkazi wa kidodi baaa ya kumkuta na silaha aina ya shotgun isiyokuwa na namba, mtutu 1 wa riffle, mitutu 7 ya shotgun na risasi 4 zilizohifadhiwa kwenye nguo na kufichwa pangoni.

Amesema, mwanaume mwingine mwenye umri wa miaka 52 alikamatwa desemba 25 katika tarafa ya Vigoi wilayani Ulanga akiwa nasilaha aina ya shortgun yenye namba 0648 bila kuwa na kibali cha umiliki aliyokuwa ameihifadhi chini ya kitanda ndani ya chumba anachoishi.

Aidha Kamanda Matei ameleeza  kuwa majina ya watuhumiwa hao yamehifadhiwa kutokana na sababu maalum ambapo wanaendelea kuhojiwa huku jitihada za kumtafua aliyekimbia zikiendelea na kwamba watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Kamanda Matei amesema, desemba 25 saa 5 asubuhi katika eneo la Upangwa kijiji cha Dodoma isanga kilichopo kata na tarafa ya masanze wilayani Kilosa mkoani hapa wafugaji wa jamii ya kimasai waliwashambulia kwa silaha za jadi na kuwajeruhi watu sita wote wakiwa ni wakazi wa kijiji hicho mara baada ya kukamatwa kwa mifugo ya mtu mmoja aitwaye Ngayoni Kimingati iliyokuwa ikiharibu mazao (mahindi).

Kamanda Matei amewataja majeruhi hao kuwa ni pamoja na na Augustino Mtitu (35) aliyechomwa na mkuki mdomoni na kutokea shingoni, George Andea (68) aliyepata jeraha la kichwani, Yohana Wisa (26) aliyejeruhiwa mkono wa kulia, Mathayo Elia (34) aliyejeruhiwa kichwani na maumivu bega la kushoto, Josephat Mtitu (55) aliyepata maumivu ya begani na ubavu wa kushoto na Paulo Thomas (56)aliyepata maumivu kwenye mbavu na mkono wa kushoto.

Amesema, majeruhi watano walitibiwa na kuruhusiwa huku Augustino Mtitu akiendelea kupata matibabu katika hospitali ya Rufaa mkoani hapa huku hali yake ikiendelea vizuri.
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment