Na Mwandishi Wetu
KLABU ya Azam imemsimamisha Kocha Mkuu, Zeben Hernandez raia wa Hispania pamoja na wasaidizi wake sita kufuatia mwenendo mbovu katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo leo jioni na kuahidi kutoa taarifa kwa makocha watakaochukua nafasi za makocha hao kutoka Hispania.
Azam imefanya maamuzi hayo huku ikiwa kesho itashuka uwanjani kuvaana na Tanzania Prisons mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam huku wakiwa na kumbukumbu za kupata sare mbili mfululizo kwenye uwanja huo.
0 Michango:
Post a Comment