KIONGOZI
wa Tume ya Uchaguzi Gambia amemtangaza mgombea wa upinzani Adama Barrow, kuwa
mshindi wa uchaguzi wa urais wa mwaka 2016.
Adama
Barrow alipata kura 263,515 huku Rais Yahya Jammeh akipata kura 212,099.
Mwandishi
mmoja wa habari kutoka shirika la Reuters anasema kuwa amezungumza na Adama
Barrow aabaye amemuambia kuwa anasubiri simu ya kukubali kushindwa kutoka kwa
bwana Jammeh.
Yahya
Jammeh ameitawala Gambia kwa miaka 22
Waziri
wa masuala ya ndani nchini Gambia na mkuu wa polisi wamehutubia taifa wakitaka
kuwepo utulivu.
Mkuu wa
tume ya uchaguzi nchini Gambia amewaambia waandishi wa habari kuwa Rais Yahya
Jammeh ambaye ameitawala nchi kwa miaka 22 baada ya kuingia madarakani kwa njia
ya mapinduzi atakubali kushindwa.
0 Michango:
Post a Comment