IKIWA ni siku moja baada ya maadhimisho ya Ukimwi Duniani kufanyika nchini, imebainika kuwa maambukizi ya virusi vya Ukimwi yameongezeka nchini.
Takwimu zinaonesha kwa sasa maambukizi ya Ukimwi kwa Tanzania bara ni kwa asilimia 5.3.
Kiwango hiko kinapanda huku uwezo wa serikali katika utoaji wa madawa kufubaza makali ya virusi hivyo ni kwa asilimia 50 ya wagonjwa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema katika ongezeko hilo wanawake wanaongoza kwa asilimia 6.2 kulinganisha na asilimia 3.8 ya wanaume walioathirika.
Mwalimu amesema kuwa kati ya wanawake 100, sita kati yao wanamaambukizi na katika idadi hiyo kwa wawanaume wanne wameathirika.
“Mwelekeo wa kupambana na ugonjwa huo ni kufikia malengo ya duniani kuutokomeza ifikapo 2030, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloratibu mapambano shidi ya ukimwi (UNAIDS) limeweka malengo ya muda kati ya tisini tatu (90-90-90)” amesema Mwalimu.
0 Michango:
Post a Comment