JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limefanikiwa kukusanya jumla ya Sh. 878.67 millioni kupitia faini za makosa ya usalama barabarani kwa kipindi cha siku nne, ambapo idadi ya magari yaliyotozwa faini hizo ni 9,817.
Jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 586 kwa makosa mbalimbali ikiwemo unyang'anyi wa kutumia silaha, kuvunja nyumba na kuiba na kucheza kamari mara baada ya kufanyika msako mkali.
Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es salaam, CP Simon Sirro amesema kuwa, oparesheni ilifanyika katika maeneo ya Buguruni na Magomeni ambapo watuhumiwa 257 walikamatwa, huku watuhumiwa hao wakikutwa na silaha ndogo ndogo kama vile visu na bisibisi ambapo lita 50 za Gongo nazo zilikamatwa.
Jeshi hilo pia kupitia kikosi kazi chake cha kupambana na ujambazi wa kutumia silaha limefanikiwa kuwakamatwa wezi wa magari na gari lililoibiwa baada ya majambazi kuvamia bar na kufanikiwa kuiba gari.
0 Michango:
Post a Comment