//
Ads

Kwa hili Dawasco Mlandizi ichunguzwe

Barua ya msomaji
MWAKA 2010 baada ya zoezi la kufungiwa mabomba ya mchina kupitia kampuni ya Dawasco kukamilika hapa Mlandizi wilayani Kibaha Mkoani Pwani tulitakiwa kulipia huduma hiyo Tsh 5000 kwa kila mwezi.

Malipo yalitakiwa kufanyika bila kuangalia ni wingi gani wa maji mtumiaji ametumia yaani haikujalisha umetumia maji mengi au machache malipo yalitakiwa yawe hivyo.

Wananchi tulikubaliana na hilo lakini baada ya miezi michache huku wakitueleza kuwa tuendelee kusubiri kila mtu aanze kulipia kiwango husika tukaletewa bili zinazoonesha kwamba miezi yote tuliyolipa pesa haikuwafikia ndipo tukawa tunaendelea kuandikiwa kwamba tuna madeni kila wanapoleta bili zao za mwisho wa mwezi.

Tulitakiwa kulipa madeni hayo na tukalipa lakini bado tunaumizwa na kuambiwa kuwa bado tunadaiwa wakati tumeshalipa na kwamba miamala tuliyoitumia kulipa bado hawaitambui jana tulikutana na Mbunge tukamkumbusha hilo mbunge  wa Kibaha Vijijini, Abuu Juma akasema tumuone mtu anayeitwa  Eliudi katika ofisi za Dawasco.

Nilitoka kama mmoja wa wahanga kufuatilia suala hilo, nilionana naye kumueleza  na kumuonyesha ile kalatasi alipoiangalia adai haina saini na nilipojaribu kumuonesha akasema yeye sio muhusika.

Nilimuona  mtu anayehusika na  pesa huko sikupata ufumbuzi wa jambo langu baadae nilipohoji alikuwa dada mmoja naye ni mfanya kazi akaniambi kwamba nimeshaibiwa na sina wa kumshitaki maana huyo niliyekuwa nampatia pesa simjui na kwamba nikaandike barua ya madai.

Sasa ninashindwa kuelewa  kama ofisi  inamwajili mfanya kazi apokee malipo ya wateja halafu pesa hizo zisemwe hazikufika?


Inawezekanaje wasiwe na kumbukumbu wakati tulikua tunalipa pesa hizo ofisini hapo na wakipokea  pesa wanao pokea wanasaini na kudaiwa mteja hapa kuna tatizo la kulinda masilahi ya watu na kutuibia sisi walala hoi naomba  itumwe tume ya uchunguzi watusaidie swala hili   kuna majipu hapa dawasa Mlandizi jamani.  

Ni mimi
Abdallah Ally, Mlandizi
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment