Msanii wa muziki wa Hip Hop, Kala Jeremiah amedai atafanya jitihada za kumtafuta Dk Louis Shika ili apate madini kutoka kwa mzee huyo ambaye anadaiwa kuwa ni msomi wa udaktari.
Akimzungumzia 'tajiri mtata' , Kala alisema mzee huyo anaonekana kuwa ni msomi mkubwa na tayari ana mambo mengi amejifunza akiwa nje ya nchi alipokuwa alisoma na kufanya kazi enzi za ujana wake.
“Binafsi nitamtafuta kwaajili ya kujifunza, yule ni mzee mwenye mambo mengi, aliyopitia, ni mafunzo tosha kwa vijana kama mimi na wengine. Kwahiyo nitamtafuta ili nijifunze,” alisema Kala.
Kala alidai kwa kuwa nyimbo zake ni za kijamii zaidi, ataangalia uwezekano wa kumtumia katika baadhi ya project zake kama akipata nafasi.
Pia rapa huyo aliitaka serikali kumtumia mzee huyo katika Tanzania ya Viwanda kwa kuwa anaonekana ana mambo mengi ambayo anayafahamu.
Dk Louis Shika hivi karibuni aliingia kwenye headline baada ya kushindwa kutoa asilimia 25 ya mnada wa nyumba za Lugumi muda mchache baada ya kushinda mnada huo na kudai pesa zake zipo Urusi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 Michango:
Post a Comment