MBUNGE wa Geita Joseph Musukuma leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama Hakimu Mkazi Geita, kujibu tuhuma zake zinazomkabili, baada ya kushikiliwa na polsi tangu jumapili ya wiki iliyopita.
Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo, amethibitisha kumpeleka Mahakamani mbunge huyo, ambaye anatuhumiwa kuhusika na kuratibu vurugu katika mgodi wa GGM mkoani humo.
“Wamepelekwa Mahakamani asubuhi hii”, amesikika Kamanda Mwabulambo akisema.
Mbunge huyo pamoja na baadhi ya wadiwani na wananchi, walikamatwa na polisi kwa kufunga njia inayoeleka kwenye mgodi wa GGM na kuleta vurugu, kushinikiza mgodi huo kulipa dola milioni 12.
0 Michango:
Post a Comment