IGP Simon Sirro |
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro juni 6 alifanya mazungumzo na
wazee pamoja na viongozi wa dini wilayani Kibiti mkoani Pwani ili kubaini
wahalifu wanaotekeleza mauaji ya watu wilayani humo na kusema vyovyote
itakavyokuwa lazima watawarudisha kwenye msitari.
IGP
Sirro alisema kupitia mazungumzo hayo tayari amepata taarifa za wahalifu hao
ingawa ni mapema kuziweka wazi ila amewahakikishia wananchi kuwa wahalifu wao
ni lazima watapatikana.
Kubwa
ni kwamba wazee wetu wa Kibiti wametueleza taarifa nyingi sana na mnavyojua
hawa wahalifu wanaishi ndani ya Kibiti, ndani ya Ikwiriri, kwa hiyo wazee wetu
wamejaribu kutueleza ni wapi tunaweza kuwapata na chanzo cha mambo yote haya alisema
IGP Sirro na kuongeza kuwa
“Kwa hiyo kimsingi mambo
mengine mengi ni ya kipelelezi ambayo siwezi kuyasema kwa sasa, lakini kikubwa
wametupa dira, muelekeo kwa maana kwamba wale ndugu zetu au maadui zetu kwa
lugha nyepesi tumepata njia nzuri ya kudeal nao. Kwa hiyo nitume salamu kwao kwamba
waendelee kukimbia lakini njia ya muongo ni fupi na mwisho wa siku
tutawarudisha kwenye mstari"
0 Michango:
Post a Comment