Msanii wa miondoko ya 'hip hop' nchini,
Godzilla amefunguka kwa kuwachana wasanii wenzake wanaoishi Ukonga Jijini Dar
es Salaam kwa kuwaambia ni miyeyusho japokuwa ni ndugu zake wa kipindi kirefu
na bado anawalea.
Zilla amesema hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV
baada ya kuulizwa chanzo cha ugomvi wake yeye na msanii Nikki Mbishi
pamoja na Wakazi kwa kudai kwamba hawajagombana kama watu wanavyodhania
ila tatizo ni kwamba hamuelewi namna alivyo.
"Nikki
'is my friend' tumefanya kazi kwenye nyimbo yake, 'i don't know'
sijui kitu gani kimetokea lakini 'we still friend. Mimi sina tatizo kwa sababu
kama ingekuwa chochote kimetokea watu tusingefanya kazi pamoja, lakini imekuwa
'too much'.. Unajua watoto wa Ukonga wengi wanakuwa miyeyusho miyeyusho lakini
ni ndugu zangu wakina Wakazi, Nikki tunawalea tutafanyaje wanetu hao" alisema Godzilla kupitia eNewz ya EATV.
0 Michango:
Post a Comment