Tazama baadhi ya picha bora kutoka barani Afrika na zile za Waafrika wakiwa sehemu mbali mbali duniani.
![]() |
Mchuuzi akiwauzia wapita njia na wenye magari panya waliochomwa eneo la Salima, Malawi, siku ya Jumatatu. Panya waliochomwa wanapendwa sana na watu nchini Malawi na biashara yake hunoga sana hasa vijijini. |
![]() |
Siku hiyo hiyo mwendeshaji pikipiki wa mashindano ya pikipiki wa Afrika Kusini aliwatumbuiza watu waliofika kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya kuwepo kwa jimbo la Lagos, nchini Nigeria. |
![]() |
Siku hiyo hiyo kobe huyu wa aina ya 'ploughshare' aliokolewa nchini Malaysia baada ya kusafirishwa kinyemela kutoka Madagascar. Maafisa walipata kobe 330. Kobe hao walikuwa wamewekwa kwenye masanduku amabayo yalidhaniwa kusafirisha mawe kutoka uwanja wa ndege wa Antananarivo, nchini Madagascar. |
0 Michango:
Post a Comment