Edward Lowassa |
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa ametaja mambo matano yanayomkasirisha ambayo yanafanywa na Serikali ya Tanzania huku akiionya CCM kuwa ipo siku upinzani utatawala nchi.
Waziri Mkuu huyo wa zamani, alisema hayo jana wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake Mikocheni wilayani Kinondoni.
Lowassa alitaja mambo yasiyompendeza kuwa ni pamoja na kuzuiwa kwa kongamano la kujadili demokrasia ambalo lilipangwa kufanyika jana, sakata la vyeti feki na Serikali kukaa kimya kuhusu mafuriko.
Mengine ni kupanda kwa bei za vyakula na Rais John Magufuli kutohudhuria tukio la kuaga miili ya wanafunzi waliopata ajali wilayani Karatu mkoni Arusha.
Juzi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la Demokrasia lililoandaliwa na Chadema, Makongoro Mahanga alitangaza kuwa lingefanyika jana katika Ukumbi wa Arnatouglou, Ilala na wanasiasa wakiwamo viongozi wa CCM na wananchi wa kada mbalimbali wangeshiriki.
Hata hivyo, siku hiyohiyo jioni, CCM ilitoa taarifa ya kukanusha viongozi wake kualikwa katika kongamano hilo.
0 Michango:
Post a Comment