Na Mwandishi wetu
BURUNDI ilundwa kama
ufalme ulioongozwa na Watutsi waliotawala Wahutu. Lakini kabla ya ukoloni
mipaka kati ya makundi hayo haikuwa imara mno; Wahutu matajiri katika utumishi
wa mwami waliweza kupanda ngazi na kuwa Watutsi na pia Watutsi maskini waliweza
kushuka ngazi na kuhesabiwa kati ya Wahutu, hasa baada ya kuoa au kuolewa na
mtu wa upande mwingine.
Uhusiano wa makundi
hayo ulifanana zaidi na ule wa matabaka si wa makabila tofauti, pia kwa sababu
lugha ilikuwa moja kwa wote.
Utawala wa kikoloni
uliimarisha mipaka kati ya makundi hayo mawili maana kila mtu aliandikishwa na
kupangwa katika moja kati ya makundi hayo. Pia Wabelgiji walipendelea Watutsi
na kuangalia wapate nafasi zote za uchifu ambako walipaswa kutoa kibali.
Kuhamia katika kundi lingine kulikwisha. Uhusiano kati ya makundi ulianza
kufanana zaidi na ukabila.
Mwishoni mwa ukoloni
Wabelgiji walibadilisha msimamo na kupendelea Wahutu.
Katika hali hiyo
Burundi ilikaribia uhuru. Vyama vya siasa viliundwa vilivyofuata ugawaji wa
kimbari kati ya Watutsi na Wahutu. Mapigano ya kwanza kati ya Wahutu na Watutsi
yalitokea mwaka 1959 kabla ya uhuru yakakomeshwa na Wabelgiji.
Baada ya uhuru katika
Burundi, kinyume na Rwanda, utawala ulibaki upande wa Watutsi kwa sababu jeshi
lilikuwa mikononi mwao. Vipindi vya mashambulio kati ya vikundi vilifuata.
Mwaka 1972 malaki ya
Wahutu waliuawa na jeshi la Kitutsi waliolenga hasa Wahutu wenye elimu.
Mwaka 1993 uongozi wa
Kitutsi ulikubali tena uchaguzi huru ambako Mhutu Melchior Ndadaye alichaguliwa
kuwa rais. Alipouawa na wanajeshi Watutsi malaki ya Watutsi waliuawa na Wahutu
wakali.
Kipindi kilichofuata kilikuwa cha Vita ya wenyewe kwa wenyewe katika sehemu mbalimbali za nchi.
Tangu mwaka 1995 Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa zilijitahidi kujenga mapatano kati ya vikundi. Marais na wanasiasa walioshiriki katika jitihada hizo walikuwa pamoja na Julius Nyerere, Boutros Boutros-Ghali, Nelson Mandela, Thabo Mbeki na rais wa Marekani Bill Clinton.
Kipindi kilichofuata kilikuwa cha Vita ya wenyewe kwa wenyewe katika sehemu mbalimbali za nchi.
Tangu mwaka 1995 Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa zilijitahidi kujenga mapatano kati ya vikundi. Marais na wanasiasa walioshiriki katika jitihada hizo walikuwa pamoja na Julius Nyerere, Boutros Boutros-Ghali, Nelson Mandela, Thabo Mbeki na rais wa Marekani Bill Clinton.
Mapatano yalifikiwa na kusainiwa mwaka 2000 na washiriki karibu wote huko Arusha. Majadiliano yaliendelea hadi mwaka 2003 hatimaye vita ilisimamishwa. Mapatano yaliyofikiwa yanasema ya kwamba Watutsi pamoja na Watwa, ambao ni asilimia 15 za wananchi, watakuwa na asilimia 40 ya nafasi kwenye bunge na ya kwamba jeshini kila upande utashika asilimia 50 za nafasi. Pia kwenye senati ya bunge kila upande utakuwa na asilimia 50. [8]
Rais atachaguliwa na wananchi wote lakini mapatano yalisema rais wa kwanza atachaguliwa na bunge.
Hali ya kisiasa hivi sasa sionzuri lakini Hii Ndiyo Orodha ya Maraisi wa Nchi ya Burundi..
![]() |
28 Novemba 1966 – 1 Novemba 1976 Michel Micombero |
![]() |
2 Novemba 1976 – 3 Septemba 1987 Jean-Baptiste Bagaza |
0 Michango:
Post a Comment